Skip to main content

SULUHISHO KWA WANAUME WANAOFIKA KILELENI HARAKA


Usidanganyike na kuanza kutafuta dawa, dawa unayo mwenyewe. Chanjo kikuuu cha kumwaga haraka na kukosa kurudia mara ya pili ni kuwa na woga au hofu au wasiwasi, pili ni ugonjwa na tatu ni uzoefu. Kama hujazoea tendo la ndoa basi ni dhahiri kila wakati utaona nyota nyota tu. Cha kufanya kama umeoa hakikisha unarudia mara kwa mara. Sasa rafiki yangu moja aliniambiya hawezi rudia mara ya pili kozi anakuwa amechoka kabisa na hamu ye tendo inakuwa imeisha, amelowa jasho na anasikia aibu kwa kufanya kitendo chini ya kiwango. Ndugu wewe ni mwanaume, lazima uonyesho udume wako. Kama unasikia woga na wasiwasi na kutokwa jasho basi hilo ni tatizo dogo, ondoa wasiwasi jiamini, kujiamini kunaleta nguvu na kuondoa hofu mashaka na wasiwasi. Sasa huwezi jiamini kama hujajiandaa na kujiandaa ni kujifunza.
Kwanza hakikisha unamiliki tendo na kutokufikiria kufika kileleni haraka, ukifila kileleni mapema usijali rudia tena.
Hofu wasiwasi na mashaka ndio huleta kutokujiamini, na kutokujiamini ni mataokea ya gap (kukosa maarifa na elimu) kati ya unachokifanya na kile unachodhania unatakiwa kukifanya (gap between actual results and expectation). Ikiwa unafika kileleni mapema na unauhakika si kwa sababu ya woga wasiwasi na mashaka basi jitahidi kufanya tendo la ndoa mara kwa mara ili upate uzoefu. Na kama utakuwa umefanya hivi na bado hupati matokeo mazuri basi huo ni ugonjwa wa aidha kisukari au pressure au figo au ini. Fika hospitalini pima na pata dawa.

NINI CHA KUFANYA UCHELEWE KUFIKA KILELENI – Jinsi mwanadamu alivyoumbwa ni kwamba ili mwanaume ufike kileni inatakiwa kuwe na msuguano wa kutosha kati ya uke na uume, ili ya kwamba utokee msisimko mkubwa utakaowezesha kuvuta mbegu za kiume kutoka kwenye makorodani hadi kwenye uume na kuingia ukeni. Sasa ikiwa mbegu zako zinatoka haraka sana hata bila ya msuguano mkubwa kati ya uke na uume basi  hapo kuna shida sana, kuna wanaume ambao wana nguvu za kiume kawaida tu lakini tatizo lao wanawahi kufika kileleni, mwanaume mmoja wa Mwanza aliniambiya yeye akigusa tu anasikia vitu vinanyefua nyefua na mara moja amekojoa, mke wake amemchukia mpaka siku hizi amemsamehe. Nilivyojaribu kumdadisi huwa anawaza nini wakati anataka kufanya tendo la ndoa ndio majibu ninayokupa hapa chini – Uzuri hawa watu waliamua kujitoa fahamu na mke wake akachukua simu na kuniambia mume wake anachanganyikiwa kwa sababu yeye mwanamke anajoto kubwa sana, na ni mweupe sana kama mzungu sasa mwanaume akimsogelea tu mwili unakuwa wa joto kuliko maelezo, uume unasimama haraka sana, na akigusa tu mambo kwisha. Bahati yao wana mtoto mmoja wa kiume, nilivyomdadisi mwanaume anasema kuna siku moja moja huwa anabahatisha kuingia na kusukuma mara mbili au tatu hivi na kisha manii hutoka kwa nguvu sana kama maji ya presha ya bomba.

Hawa ndugu kwa sasa wanaendelea vizuri ingawa bado hawajafikia ufanisi mkubwa – Nilichowashauri wote wawili na ambacho baada ya kukifuata kikawasaidia – Bwana mkubwa nilimwambia ajaribu kufanya tendo la ndoa kwa ile staili anayodhania anaipenda sana, na kwa mujibu wake ni kwamba angependa sana mwanamke amkalie. Na ndipo waliamua kufanya hivyo, kwa muda kama wa week nzima kijana kama kawaida yake ni kuwahi tu na ilipofika week ya pili akawa anaweza kurudia mara ya pili, na ndio ukawa mwanzo na ufunguo wa kujua kulikoni kwenye tendo la ndoa. Week ya tatu ilipofika wakawa sasa cha kwanza haraka kama kawaida ila cha pili kinachukua muda kidogo, naamini baada ya mwezi wanandoa hawa watakuwa ma-expert na mwanaume huyu atajuta kwa nini hakujifunza mapema. Sheria ni kuhakisha uume umesimama kabisa 100% na umekuwa mgumu kabisa, usiwe legelege ndipo umuingilie mwanamke, pili punguza presha yote kabla hujaingiza uume, hakikisha mapigo ya moyo yako chini kiasi, wakati huoho angalia mwenzako naye mapigo yake yawe juu kidogo (ameshakolea). Na staili hii inamsaidia mwanaume kuondoa ule msisimuko ulioko kwenye kichwa cha uume na kisha kuuweka mgumu tayari kwa tendo la pili, ikiwa mwanamke atakuwa mjanja pia anaweza jitahidi kuubana uume kwa kutumia uke wake kama anaukamua vile – ili kuhakisha uume unaondoa ule msisimuko feki au tunasema msisimuko wa kimawazo. Pia mwanaume ajaribu kusukuma uume taratibu na kwa kutumia nguvu zaidi ya mwili kuliko uume, ile hali mwanamke akiwa ana slide mbele na nyuma badala ya kupanda juu na kushika chini -angalia mfano hapa. Hii inasaidia kukomaza uume na kuufanya mgumu zaidi. Mpaka hapo nadhani utakuwa umeelewa ya kwamba kwanza lazima, ukiondoe kile kinachokufanya umwage haraka, ondoa hofu na mashaka, kubali ya kwamba unawahi mapema na mkeo ajue yakwamba unania ya kurekebisha hilo, chakula ni muhimu pia, kisha sasa jifunzeni mwenyewe kujikawisha (kujizuia unapokaribia kufika kileleni kama vile unavyojaribu kubana mkojo) – sio kitu kigumu ila wanaume wengi wanataka yaani akianza leo basi kesho iwe ameshafanikiwa, sio rahisi hivyo ndugu kwa sababu ya mazoea yako ya mwili na akili.

DAWA ZIPO ZA KUKAWISHA KUFIKA KILELENI – Lakini na zenyewe zinafanya kazi vizuri ikiwa na wewe utajisaidia na kujifunza nini cha kufanya, ikiichia dawa kazi asilimia mia, nakuhakikishia utapomaliza dozi unarudi kule kule kwenye cha kwanza haraka kimefyatukaDawa nyingi zinafanya kazi kwa mtindo huo huo wa kuondoa ule utamu na hisia za haraka kwenye kichwa cha uume, dawa zinaweza kuwa ni zakupaka mafuta, sindano, vidonge au juice. Dawa nzuri kwa sasa ni za tiba mbadala angalia hapa baadhi ya mifano yake.


NINI CHA KUFANYA KUMWAHISHA MKEO AFIKE KILELENI – Mbinu moja nzuri sana na ya tangu zama za Adamu na Hawa ni kuhakisha ya kwamba mkeo anafika kileleni kwanza au tuseme kuhakisha ya kwamba mkeo anakuwa wa kwanza kupata msisimuko na kuwa tayari kwa tendo. Ndugu mwanaume ni ngumu kuelezea lakini nitajitahidi kadri ya uwezo wangu. Inapofika wakati wa kutaka kuanzisha tendo la ndoa, kwanza jaribu  kumpa nafasi mkeo ya kukuandaa wewe na unapokuwa umehisi uko vizuri, usimwingilie badala yake wewe anza kumwandaa yeye. Faida yake ni kwamba mwili wako unaanza kutulia na kuzoea kuelekea kwenye kufanya tendo la ndoa, hakikisha unaendelea kumwandaa mpaka yeye mwenyewe anaonyesha dalili za kutaka kuingiliwa, hapo utakuwa umemaliza. Inafurahisha sana kama utakuwa umeweza kufikia kiwango hiki kwani inakupa ujasiri wa kujua ya kwamba kazi unayoifanya inazaa matunda, hawezi chukua zaidi ya dakika 5 atakuwa amemaliza. Ofcourse pamoja na mambo mengine inafaa muwe mnapendana na hakuna ugomvi baina yenu. Jambo lingine ni wewe kujitahidi kufanya tendo la ndoa katika siku zake za uzazi yaani kuanzia siku ya 10 hadi ya 18 katika mzunguko wake wa uzazi, kumbuka hizi ni siku za uzazi na kwa hiyo msipotumia kinga atapata mimba kama huna mpango wa kutungisha mimba. Kama mnaujua vizuri mzunguko wa hedhi wa mke wako basi unaweza fanya siku moja au mbili baada ya yai kupevuka ili kuepukana na mimba. Ikiwa unataka kujua namna nzuri ya kuhesabu siku za uzazi na mzunguko wa hedhi wa mke wako basi tembelea hapa.
Kuna maarifa mengine mengi tu lakini nimejaribu kuweka mfano wa kitu rahisi kukubalika na kila mmoja

MESSAGE KIDOGO INAWEZA SAIDIA (bofyahapa- Hapa ni kwa wale wanaume wenye muda na wasiokuwa na usingizi wala stress za kazi. Yaani unatumia muda kidogo zaidi ya dakika 10 hadi 15 kumfanyia message mke wako, na lazima uanze na sehemu zilizo na msisimuko wa kawaida kama mabega, mgongo na tumbo  na kisha sehemu zenye msisimuko wa kati kama mapaja na maziwa (bila chuchu) na kisha kumalizia na uke. Massage ni nini? Massage mara nyingi hutumika kwa ajili ya kustarehesha mwili na kuutuliza hasa kutokana na mwili kuchoka sana kutokana na uchovu wa akili na mambo mengine kama stress na kipanda uso. Sasa kuna massage za kawaida na romantic massage, ikiwa utaamua kufanya romantic massage basi mkeo lazima ajue nini unachokifanya. Romantic massage ni mbinu mojawapo ya kuamsha hamu ya mwanamke kwa kutumia mikono zaidi na kupapasa kwa namna ya kukandamiza sehemu tajwa hapo juu. Massage nyingine inayojitegemea kabisa ni foot massage, au ku-message mguu tu, kwa kiasi kikubwa mguu unasisimua sana kwa hiyo inatakiwa uende taratibu sana kwa kuanzia na sehemu zenye msisimuko kidogo kama kisigino na kisha kumalizia na sehemu yenye msisimuko mkubwa sana katikati ya mguu yaani wayo. Faida za massage kama kawaida ni kuongeza msisimuko, kuongeza hamu, kuwahisha mwanamke kufika kileleni, na pia kukusaidia wewe mwanaume mwili wako kuwa mtulivu kisaikolojia na hivyo kukupa nafasi ya kuimarika uume wako na kuwa mkubwa na mgumu ndio usimwage haraka.

Maandalizi ya romantic massage yanweza anzia wakati wa kuoga ambapo unatakiwa umwogeshe tangia kuanza kupaka sabuni hadi kujikausha na kuvaa nguo, na kisha andaa mishumaa au taa iwe hafifu labda na mziku mwepesi kidogo, kiasi ya kwamba mtu aliyepo mita kama 4 ivi hawezi sikia, mashuka mekundu pia yanaweza saidia, mafuta kidogo yanaweza saidia hasa ikiwa mkeo ana mwili mgumu. Romantic massage idumu kwa muda mfupi kama dakika 15 hivi. Wengi waliojaribu mbinu hii hawajafika zaidi ya dakika 7 unakuta kila mtu tayari anataka na ndio inakuwa mwisho wa massage na mwanzo wa tendo la ndoa. Ina faida kubwa sana hasa kama mwanamke ana uke mkavu, anachelewa kufika kileleni au pale mwanaume anapokuwa na uume unaolegea na pia anawahi kufika kileleni, romantic massage inakuwa ni masaada mkubwa sana.

Kumbuka ya kwamba mbinu zote zinazotumika kumsisimua mwanamke zina sifa moja tu kuamsha ubongo na kisha ubongo kupeleka taarifa sahihi katika viungo husika. Kwa hiyo unapobusu, unapogusa, unaposugua, unapoguna na kupapasa taarifa zote zinaufikia ubongo na ubongo unazipeleka taarifa hizo kunakohusika. Wayo una milango ya fahamu ya moja kwa moja na ubongo, ukitekenya wayo hadi ile kelele ya wayo unaisikia iketekenya kwenye ubongo, mapaga na mabega vile vile. Chamsingi ni kuwa na ufundi na uthubuti wa kujua nini cha kufanya wapi na saa ngapi, lakini pia kuwa makini na uangalie maendeleo ya unayemfanyia massage yaani isiwe too shalow na isiwe too much.

0752-693 692 au 0655 580 788

Comments

  1. Asante sana nimekuelewa mwanza mwisho namini itatusaidia wanaume wengi. Mung akubariki

    ReplyDelete

Post a Comment