Sheria ya kawaida ya massage.
1- Ichukue dakika 30-60, mahali tulivu na salama
2- Anayefanyiwa massage alale chali au kifudifudi akinyooka
3- Anayefanyiwa massage afumbe macho na kuwa kimya
4- Uwekwe mziki laini na kuwasha mshumaa.
5- Tumia mafuta kulainisha mwili na mikono.
6- Ili kuzuia matandiko/mashuka kuchafuka tandika taulo.

#foreplay #kumwandaa #kujiandaa, masaji kwa kiswahili rahisi #kuchua
#inaweza_saidia_wale_walioshindikana_kupata_hamu_yatendo_landoa
#inaweza_saidia_wale_walioshindikana_kupata_hamu_yatendo_landoa
Ndio kuna masaji za wapendanao jaribu mojawapo, hutakuwa kama zamani, utarelax na kumfikiria zaidi mwenzako kuliko kujifikiria wewe kwanza. Katika somo moja lililopita tulifundisha “give yo shall be given” na hapa suala la masaji lina mashiko sana. Mara nyingi linapokuja suala la tendo la ndoa basi akili ya wanandoa ni kuwa mwanamke ndio anatakiwa aandaliwe, kuna ka-ukweli flani kulingana na historia na mapokeo ya vizazi vilivyopita. Lakini ka-ukweli hako sio lazima kawe kweli daima.
Zamani kidogo watu wenye uvimbe hasa utokanao na kansa walikuwa wanavukiziwa mvuke sehemu iliyovimba na kisha kunywa dawa au kusemea maneno kadhaa (mara nyingi ya kishirikina). Kisayansi hapo walikuwa wanachangamsha misuli na mishapa ya damu ili damu ipite haraka, ingawa la ushirikina halina ukweli kisayansi. Haina tofauti sana na Massage ya kizungu. Unaweza kuwa umewahi kusikia habari ya “body massage” ambayo ni kitu kigeni kidogo Africa, massage hufanywa ili kuondoa uchovu wa mwili utokanao sana sana na kufanya kazi nyingi za kukaa maofisini, kuwa na mawazo mengi na pia kwa ajili ya kuamsha mishipa ya damu na milango mbalimbali ya #hisia iliyolala na kuziba. Massage ni tofauti kidogo na “kutomasa au kupapasa”. Massage hufanywa sehemu mbalimbali za mwili na kwa kiasi kikubwa huepuka sehemu za kusisimua mwili kama vile maeneo karibu au sehemu za siri na chuchu. Massage hufanywa kwa kuchua (kukandamiza na kusuuza na kuachia) sehemu mbalimbali za misuli hasa muscles/misuli za mwili. Unaweza tumia mikono, ngumi, miguu, kiwiko cha mikono au visigino vya mguu ilimradi lengo kuu la kuchua mwili lifikiwe. Massage inafanywa kwa kutumia mafuta maalumu ya mzeituni, laventa na mengineyo. Lengo hasa la mada hii siyo kuelezea namna ya kufanya massage kifasaha bali kukuelimisha ya kwamba massage za wapendanao zipi na unaweza kuifanya nyumbani au ukaenda massage room wewe na mwenzako mkafanyiwa wote kwa pamoja. Katiak mada hii nitaongelea massage ya kufanyiana wanandoa/mahusiano nyumbani mkiwa peke yenu.
Kuna aina nyingi sana za massage na zenye majina mbalimbali na sababau mbalimbali (deep tissue, swedish na aromatherapy) lakini katika ukurasa huu nitaelezea vipengere vitatu ambavyo ni vizuri kwa wanamahusiano kwa kuwa lengo kuu ni kurekebisha mfumo wa hisia, kustarehesha, kupumzisha na kuamsha akili. Ingawa lengo kuu la massage zote sio kuamsha hamu ya tendo la ndoa katika hivi vipengere vitatu hapa chini lengo ni maandalizi ya kufanyika tendo la ndoa muda flani na sio wakati huohuo, ingawa kama itafanyika muda huo huo pia sio mbaya.
Sheria ya kawaida ya massage.
1- Ichukue dakika 30-60, mahali tulivu na salama
2- Anayefanyiwa massage alale chali au kifudifudi akinyooka
3- Anayefanyiwa massage afumbe macho na kuwa kimya
4- Uwekwe mziki laini na kuwasha mshumaa.
5- Tumia mafuta kulainisha mwili na mikono.
6- Ili kuzuia matandiko/mashuka kuchafuka tandika taulo.
1- Ichukue dakika 30-60, mahali tulivu na salama
2- Anayefanyiwa massage alale chali au kifudifudi akinyooka
3- Anayefanyiwa massage afumbe macho na kuwa kimya
4- Uwekwe mziki laini na kuwasha mshumaa.
5- Tumia mafuta kulainisha mwili na mikono.
6- Ili kuzuia matandiko/mashuka kuchafuka tandika taulo.
Hizi ni aina za massage unazoweza mfanyia mwenza wako, hakikisha unapata angalau utaalamu kidogo wa kufanya massage, pia tumia mafuta ya mzeituni kulainisha sehemu unayoifanyia massage, fuatisha mtiririko wa misuli ilivyolala ndio uchue, usugue, usage, ukandamize na kusuuza kufuata mielekeo ya misuli.
MASAJI YA #MGUU, #WAYO NA #VIDOLE (foot massage) – Mguu ni sehemu moja ambayo imejaa miishio ya mizizi ya fahamu (kwa hiyo inamsisimko mkubwa), kama utaifanyia massage/mkandamizo wa kiasi, kuanzia kwenye shingo ya mguu kuelekea vidoleni na kisha kumalizia na wayo. Gusa kwa nguvu kiasi maungio ya vidole vya miguu (kati ya pingili na pingili), na chua kwa kiasi kwenye unyayo, rudia rudia mara kwa mara.
MASAJI YA #MGONGO NA #MABEGA (Shoulder Massage) – Massage ya Shoulder/Mabega, ifanye masaji hii kwa mtindo wa kuchua. Itafaa zaidi kama utamfanyia mwenza wako ambaye yuko bize sana na kazi za ofisini za kukaa muda mrefu na kuchungulia makaratasi na kopyuta. Utaalamu ni kuanzia katikati ya mgongo juu kidogo ya makalio au yanapoanzia makalia na kuelekea mabegani kuzunguka kidogo kueleka kwenye maziwa/kifua lakini usifikie. Shingoni unaanzia chini mabegani na kuelekea juu upande wa kichwa na kuzungushia kwenya masikio.
MASAJI YA #MAPAJA (Thigh Massage) – kama sio mvumilivu unaweza usiifanye kwa sababu lengo la massage ni kukandamiza, kuchua na kusaga sio kutomasa na kuamsha hamu ya tendo la ndoa kwa haraka. Kwa hivyo mapaja yafanyiwe masage yote upande wa mbele na nyuma, kwa kusugua, kuchua na kusaga kwa kugandamiza misuli ya mapaja ikianzia chini kidogo ya kiuno kuelekea juu kidogo ya magoti
ONYO - ZINGATIA KANUNI ZA AFYA kwa kuwa kama kuna michubuko ya ngozi, upele na kucha ndefu unaweza ambukizwa ugonjwa wa mwenzako.
BONUS- Ukiona unayemfanyia massage ametulia na kulala au kuwa kati ya kulala na macho basi tambua kwa kiasi kikubwa umeipatia.
Nimatumaini yangu ya kwamba mada hii itakusaidia kitu katika maisha yako ya ndoa na mahusiano. Massage nyingi inawezekana kufanyika nyumbani sio lazima ufike spa – room. Kwa wale wanaohitaji maelezo zaidi nitafuteni inbox 0752 693 692 kwa kuwa siwezi andika kila kitu hapa mana wengine wanashare mada hizi hata kwenye magroup ya watoto.
Waooh
ReplyDelete