Kumekuwa pia na maswali mengi sana kuhusu namna ya kupanga jinsia ya mtoto. Kiu kweli hata ukipata maelezo tu hapa inakuwa ni kubahatisha tu. Mama mmoja wa kimasai ambaye kidogo ameenda shule amenielezea jinsi anavyo hangaika kupata mtoto wa kiume lakini imeshindikana, ameenda kwa waganga wa kila namna lakini hapati, amefika kwenye kila kituo cha maombi lakini hakupata(labda alikuwa na imani haba). Ni kwamba kwa sasa ana watoto wa kike watatu naangependa kupata mtoto wa kiume mmoja, na umri wake umekwenda sasa ana miaka 35. Siri sirini lakini ilimradi simtaji jina ni kwamba kila akibeba mimba anapima na akikuta wa kike anatoa mimba sasa ameshatoa mimba kama tatu hivi na alikuja kwangu kunieleza ya kwamba sasa yatosha, atakaye zaliwa ndio huyohuyo mwana wa Mungu. Wanawake wanateseka sana kutafuta watoto wa kiume kutokana na makwazo wanayoyapata kutoka kwa waume zao, wakati wanaume wengi wanatoa amri hizo na hawajishughulishi tena kutafuta suluhisho la tatizo, badala yake anamwachia mama ahangaike. HII SIO SAWA kwa kuwa kwa kiasi kikubwa anaye wezesha jinsia ya mtoto ni mwanaume na sio mwanamke.
Kumbuka jambo moja ya kwamba mwanaume ndiye anakuwa ana mbegu za kiume zenye kubeba jinsia zote za kiume (Y) na kike (X) wakati yai la mwanamke linakuwa na jinsia moja tu ya kike (X).
Ikiwa mbegu ya kiume yenye jinsia ya kike itaungana na yai la mwanamke na kutungisha mimba basi atakaye zaliwa ni mtoto wa kike na kama mbegu ya kiume yenye jinsia ya kiume itaungana na yai la kike basi mtoto atakaye zaliwa atakuwa wa kiume. Kwa mana nyingine mwanaume mwenye mbegu nyingi zenye jinsia ya kike atazaa watoto wanawake wengi zaidi kuliko watoto wa kiume. Kawaida wanaume wengi wana mbegu zenye jinsia zote, wanaume wachache sana ndio wana mbegu au za kiume tupu au za kike tupu. Na hapa sasa inatakiwa usome vizuri na ujue mzunguko wa hedhi wa mke wako, kama mkeo ana mzunguko wa hedhi wa siku 28 kwa mfano siku ya kupata mtoto wa kiume ni siku ya 14. Inafaa ufuate masharti ya kwamba usifanye tendo la ndoa kuanzia siku ya kwanza amepata bleed hadi siku ya 14 ndio ufanye. Ikiwa utafanye siku chache kabla ya siku ya 14 kuna uwezekano mkubwa utapata mtoto wa kike. Ukikosa kutungisha mimba mwezi huu unajaribu tena mwezi mwingine kwa kuwa kawaida huwa kuna kuwa na ukinzani wa kutungisha mimba.

kumbuka sheria ya jumla ya kwamba mtoto wa kiume unaweza mpata (kama vitu vingine vyote vitakuwa sawa) siku ya yai kutoka (ovulation day) au tuseme siku 14 kabla ya kupata bleed. Kwa maana ingine kama mzunguko wako ni wa siku 28 basi siku ya mtoto wa kiume ni siku ya 14 (28-14=14) na kama mzunguko wako wa bleed ni wa siku 32 basi siku yako ya mkupata mtoto wa kiume ni siku ya 18 yaani (32-14=18)
Angalia mfano huu mimi babu yangu alikuwa na wake watatu. Mke wa kwanza alizaa wakiume watupu watoto 12, na mke wa pili alizaa watoto wa kike watupu 7 na mke wa tatu alizaaa watoto mchangayiko wa kiume 2 na wakike 4 jumla sita. Katika hali ya kawaida unaweza sema hakukuwa na shida hapa, lakini kiukweli mke wa kwanza na wa pili walikuwa na matatizo flani au kulikuwa na uvutano usiokuwa wa kawaida kati yao na babu. Inawezekana kabisa uke wa bibi wa kwanza haukuwa na mazingira mazuri kwa mbegu za jinsia ya kiume kutoka kwa babu na bibi wa pili naye alikuwa na uke wenye mazingira hatarishi kwa mbegu za babu za jinsia ya kiume. Bibi wa mwisho yeye alikuwa sawa kabisa kwa kuwa aliweza kupokea mbegu za jinsia zote na kisha kutungisha mimba.
Hapa unajifunza jambo moja lazima mwili wa mwanamke ukae katika hali ya kawaida sana ili kuweza angalau kutoa wepesi wa kupokea mpango wa uzazi, huwezi kuanza kupanga jinsia ya mtoto ile hali wewe uke wako na mfumo mzima wa uzazi ni hatarishi kwa baadhi ya mbegu. Mfano kuna PH isiyokuwa nzuri, fangasi na harufu mbaya, uvimbe kwenye kizazi na kwenye mirija ya mimba, kuwa na magonjwa kama cyeast, STDs, PID na kuwa na mzunguko wa hedhi usiyo eleweka. Lazima kwanza utatue matatizo haya kabla hujafika mbali.
Tumalizie na mmasai sasa, huyo mama baada ya kumweleza kama nilivyoelezeya hapo juu alifurahi sana hasa kwa kuwa alikuwa amebeba lawama za bwana-ke na kujikuta kama vile yeye ndiye anayesababisha wasipate mtoto wa kiume, kwa hiyo sasa angalua anajua wote wanahusika. Lakini baada ya kufanya uchunguzi niligundua yule mama ni cha pombe sana, ukweli ilibidi nimshauri tu ya kwamba hawezi jua nini cha zaidi kinachomzuia kwa muda wa miaka minne anatafuta mtoto wa kiume hapati, inawezekana ni pombe. Na yeye akaafiki lakini sasa anasema mumewake wa kichaga ndio humletea kila siku bia moja mbili tatu. Ofcourse sasa hivi ni mjamzito tena, na anasema hana mpango wa kutoa hata kama ikiwa ni wa kike, yeye anasubiria yule mtoto Mungu amemwandalia, kikubwa ni kuwa alifanya tendo la ndoa siku ya mtoto wa kiume, itakuwa furaha kubwa sana kama siku hiyo atajifungua mtoto wa kiume jinsia anayoitaka yeye.
0752 693 692 au 0655 580 788
tembelea hapa ilikujua ni namna gani kufunga kunaweza kukuongezea hamu ya tendo la ndoa na nguvu za kiume.kwa elimu ya faya, uzazi na mahusiano tembelea facebook @healthpoint

Comments
Post a Comment